HUDUMA za kijamii mkoani Mtwara jana zilisimama kutokana na baadhi ya wananchi kudai kuwa wanaomboleza vifo vya watu vilivyotokea wakati wa
vurugu za gesi hivyo kupelekea huduma za kijamii kusimama.
Mmoja
 wa wananchi walioathiriwa na mgomo huo, Hilal John aliyekuwa safarini 
kuelekea Newala lakini alikosa usafiri kutokana na kumbukumbu hiyo 
alisema hatua hiyo imeathiri wananchi wa hali ya chini.
Alisema
 hali hiyo imesababisha wasafiri wanaokwenda wilaya zote pamoja na 
baadhi ya mikoa kushindwa kuondoka  kutokana na kutokuwepo kwa huduma 
hiyo kwa siku nzima ya jana.
Si hivyo tu, maduka mbalimbali nayo yalifungwa na hivyo kusababisha baadhi ya watu kukosa huduma hizo.
“Nimi
 nilikuwa naelekea Newala kwenye usaili lakini nimeshindwa kwenda hadi 
muda huu niko kituoni hakuna hata dalili ya magari zaidi ya mabasi ya 
kwenda Dar es salaam ndio yapo, hii inatufanya tushindwe kuelewa kwanini
 huu mgomo unafikia hatua ya kusimamisha safari  na huduma muhimu za 
kijamii”  alihoji John
Kwa
 upande wake Fatuma Halfani anayemiliki mgahawa katika kituo cha mabasi 
alisema mgomo huo kwa sehemu kubwa umeathiri akina mama lishe ambao 
wamekuwa wakitegemea biashara hiyo kuendeshea maisha yao.
 Alisema amekuwa akifanya biashara hiyo kwa muda lakini analazimika kupata hasara kutokana na mgomo ulipo ili kuepuka vurugu  .
Halfan
 alisema kitendo cha wananchi kuweka maombolezo ya mgomo kwa huduma za 
kijamii ambazo ni muhimu zinazowagusa wananchi wa hali ya chini ni jambo
 la kusikitisha kwa kuwa wananchi wa hali ya juu wanaendelea kupata  
huduma hizo.
Naye
 Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Mtwara George Salala alisema Mtwara ipo katika
 hali ya utulivu hivyo kuwataka wananchi kuendeleza amani iliyopo na 
kuwaonya wachache ambao watajaribu kufanya vurugu ambazo zitasababisha 
uvunjifu wa amani.
Alisema
 Jeshi la polisi linawataka waliokata leseni kwaajili ya biashara 
wafanye biashara na kwa watoa huduma sokoni wafungue maduka kwa kuwa 
hawatakusudia kuwachokoza kwa kuwa wao ni serikali na zaidi ofisi zote 
za serikali zilikuwa zikifanya kazi kama kawaida.
 “Sisi
 kama jeshi la polisi hatuko tayari kuona watu wanaingilia uhuru wa watu
 wengine hatutasita kuwachukulia hatua na kuwafikisha mbele ya sheria 
tunaitaka jamii ione madai hayo kama hayana tija ili tuweze kusonga 
mbele lakini hatuwezi kusonga mbele”  alisema Salala
 RSS Feed
 Twitter

11:27 AM
MZM


0 comments:
Post a Comment