Sunday, May 3, 2015

Rio Ferdinand akiwa na mkwewake Rebecca Ellison enzi za uhai wake
Rio Ferdinand akiwa na mkwewake Rebecca Ellison enzi za uhai wake
Rebecca Ellison ambaye alikuwa ni mke wa mlinzi wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Rio Ferdinand amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kansa kwa muda mfupi.
Rebecca alizaa watoto watatu na Ferdinand, watoto wao wanafahamika kwa majina ya Lorenz, Tate na Tia.
Habari hizi zimemdhoofisha Ferdinand wakati huu mgumu wa ligi kuu ya soka Uingereza, Ferdinand kwa sasa anapambana kwenye kikosi chake cha Queens Park Rangers kuhakikisha kinasalia kwenye likgi kuu kwa msimu ujao.

Klabu yake ya zamani ya Manchester United imeposti katika mtandao wake wa Twita ikisema klabu ipo pamoja na Rio Ferdinand ambaye mke wake amefariki dunia usiku wa jana. Ujumbe huo unasomeka hivi; “Everybody’s thoughts at #mufc are with Rio Ferdinand today, whose wife sadly passed away last night”.
Ferdinand ametoa tamko kwenye tovuti rasmi ya klabu yake ya sasa ya QPR akisema, “My soul mate slipped away last night. Rebecca, my wonderful wife, passed away peacefully after a short battle with cancer at the Royal Marsden Hospital in London”.
Hizi ni taarifa za kusikitisha sana kwa wapenda soka wote ulimwenguni hasa mashabiki wa Manchester United ambako alicheza kwa muda mrefu na kuisaidia timu hiyo kutwaa mataji tofauti ikiwemo ya ligi kuu, klabu bingwa Ulaya na mengine mengi kabla ya kuihama timu hiyo kwenda kujiunga na QPR.

0 comments: