Sunday, May 3, 2015

Tarehe May 3, 2015
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Weru Sengo katika pozi
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Weru Sengo katika pozi
Wasanii Steve Nyerere na Weru Sengo, katika pozi
Wasanii Steve Nyerere na Weru Sengo, katika pozi
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Weru Sengo anadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake Steve Nyerere, ambapo wamekuwa wakionekana sehemu mbalimbali wakila bata.
Inadaiwa kuwa badala ya kutoka katika matembezi au kula bata na mke wake, Steve, amekuwa akitoka na Weru, jambo ambalo watu wameona sio la kulifumbia macho na inadaiwa kuwa hata katika shoo ya Zari, walikuwa wote na kumuacha mke wake.
Vyanzo hivyo vimedai kuwa Steve, aweke bayana kama ameamua kuoa mke wa pili bila kumshirikisha mke wake kabla hawajamfanyia maandamano kama wanawake kutokana na mke wake kuwa mvumilivu na mtu anayejiheshimu.
Chanzo hicho kimetoa wito kwa mke wa Steve kumpenda mume wake zaidi ya mwanzo, kama amesikia au kuona kitu ni kawaida kwenye ndoa kupata majaribu, hivyo asimame kama mama na kudai kuwa lazima kama mke anajua udhaifu wa mume wake na kumtaka amkamatie hapo kwenye udhaifu bila kusahau kumuomba Mungu.
Kwa mujibu wa mke wa Steve, Suzy Cleo, amesema kuwa anashukuru kwa ushauri alioupata kutoka cha chanzo makini na kudai kuwa atahakikisha kuwa hatatikisika kama mwamba wa mlima Sayun

0 comments: