Vijana wawili wanatafutwa na jeshi la Polisi mkoani Morogoro kwa kumrushia bomu dereva wa gari la mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, David Ligazio ,Novatus Ngope (47), pamoja na kujeruhi watu wengine wanne walipokuwa kwenye sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani juzi.
Bomu hilo liliwajeruhi watu hao walipokuwa kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika katika kijiji cha Msolwa Ujamaa, Kata ya Sanje ,wilayani Kilombero, mkoani Morogoro
Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Kilombero, Lephy Gembe alithibitisha kutokea tukio hilo na kusema tukio hilo lilitokea majira ya saa 2:00 usiku wa Mei Mosi mwaka huu eneo la Kijiji cha Sanje.
Alisema vijana wawili wanaotuhumiwa kurusha mlipuko huo baada ya kuwajeruhi watu hao watano, walifanikiwa kukimbia kutoka eneo la tukio na jeshi la Polisi inaendelea kuwasaka ili sheria ichukue mkondo wake.
Kwa mujiu wa walioshuhidia tukio hile wamebainisha kwamba vijana wawili wasiofahamika walikamatwa katika eneo la sherehe hizo lakini kabla ya kupelekwa kituoni , vijana hao walifanyiwa upekuzi na askari wa mgambo, Thomas Manjole(54) ,mkazi wa Msolwa na walibainika kuwa na bomu.
Inadaiwa kuwa vijana hao walilitoa bomu hilo kiunoni na kulirusha kwenye gari la halmashauri ambalo linatumiwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo.
Bomu hilo lilipolipuka likamjeruhi dereva wake aliyekuwa ndani ya gari pamoja na wengine wanne akiwemo askari mgambo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye hakuwemo ndani ya gari aliwataja majeruhi hao ni dereva wake ,askari mgambo alikuwa akiwapekuwa vijana hao, Amos Msopole(29) na Azama Naniyunya(59) wote wakazi wa Kijiji cha Msolwa Ujumaa.
Hili ni tukio la pili kutokea mkoani Morogoro kufuatia lile lililotokea siku kadhaa zilizopita ambapo jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na mabomu pamoja na vifaa vya milipuko msikitikiti.
0 comments:
Post a Comment