Wanamuziki nchini Nigeria, Peter na Paul Okoye, wamekuwa wakikwaruzana mara kwa mara kiasi cha kuwashangaza watu kuwa iwaje ndugu wa damu wanakosana wakati wanafanya kazi kama timu.
Hatua hiyo imepelekea Peter, kuweka wazi kuwa, kugombana kwao kusichukuliwe kama kitu cha ajabu kwani nao ni binadamu hivyo kukosana kupo na hakupingiki.
Amesema kuwa kutofautiana kwao ni jambo la kawaida na imekuwa ikitokea hivyo mara nyingi lakini baadaye maisha yanaendelea.
Ameongeza kuwa huwa inatokea kutofautiana kwa hapa na pale kama walivyo binadamu wengine na baadaye kumaliza tofauti zao na kufanya kazi.
Amesema kuwa wao ni kama wanandoa walioishi kwa zaidi ya miaka 20 hivyo kukosana kupo na kama binadamu hupatana na kupanda jukwaani kufanya makamuzi kama kawaida bila watu kujua kama wamegombana.
0 comments:
Post a Comment