Saturday, May 2, 2015


  1. Ujerumani imetuma meli mbili za jeshi lake la wanamaji katika juhudi za kuokowa wakimbizi wasipoteze maisha yao katika bahari ya Mediterenia wakati wakikimbilia barani Ulaya kutafuta maisha bora.
  2. Meli ya kivita ya usaidizi Berlin na manowari Hessen za Ujerumani.
  3. Meli ya kivita ya usaidizi "Berlin" na manowari "Hessen" za Ujerumani.
  4. Meli hizo mbili meli ya kivita ya usaidizi yenye jina la Berlin na manowari inayoitwa Hessen zimeondoka hapo Ijumaa (1.05.2015) katika eneo la Pembe ya Afrika kwa kupitia Mfereji wa Suez nchini Misri kabla ya kuingia bahari ya Mediterenia.
  5. Msemaji wa jeshi la wanamaji la Ujerumani mjini Rostock ameliambia shirika la habari la Ujerumani dpa kwamba meli hizo mbili ilikuwa zinatarajiwa kutia nanga huko Souda katika kisiwa cha Ugiriki cha Crete hapo Jumamosi(02.05.2015).
  6. Amesema meli hizo zitatumika kusafrisha chakula na mablanketi kwa ajili ya wakimbizi wanaohatarisha maisha kukimbilia Ulaya kwa kupitia bahari ya Mediterenia ambapo wiki chache zilizopita mashua moja iliokuwa imebeba wahamiaji kutoka Libya ilizama na kuuwa takriban watu 800.

  7. Uwezo na majukumu
  8. Wahamiaji katika harakati za kuokolewa katika kisiwa cha Rhodes,Ugiriki. (20.04.2015)
  9. Wahamiaji katika harakati za kuokolewa katika kisiwa cha Rhodes,Ugiriki. (20.04.2015)
  10. Manowari hiyo ya Hessen ina mfumo wa rada ambao unaiwezesha kuzigunduwa mashua za wahamiaji zikiwa umbali wa hadi kilomita 40.Kwa upande mwengine meli ya kivita ya usaidizi inayoitwa Berlin ina uwezo wa kubeba na kuwahudumia watu 250 kwa siku mbili.
  11. Meli hizo zimepelewa Mediterenia kwa ajili ya shughuli hizo licha kuwapo kwa repoti kwamba shughuli zao kwa kina bado hazijafahamika.Meli hizo zilikuwa zikifanya kazi kama sehemu ya Operesheni Atalanta ya Umoja wa Ulaya kupambana na uharamia katika eneo la Pembe ya Afrika.
  12. Shirika la habari la Ujerumani dpa likikariri duru za jeshi la Ujerumani limesema meli hizo zitaendesha shughuli zake kwa kujitegemea zikiwa huru kutoka wakala wa kulinda mipaka ya Ulaya Frontex ambalo shughuli zake zimejikita kulinda mipaka ya nje ya nchi wanachama wa umoja huo na sio kuokowa wahamiaji walioko hatarini baharini.
  13. Kwa mujibu wa duru hizo za kieshi meli hizo za Ujerumani hazitokuwa na majukumu ya kujaribu kuwakamata watu wanaosafirisha binaadamu kwa magendo ambao hufaidikia na mamilioni ya dola kwa kuwatoza wahamiaji wanaotaka kukimbilia Ulaya kuepuka mizozo katika nchi zao na kutafuta maisha bora.
  14. Kipau mbele kunusuru maisha
  15. Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen.
  16. Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen.
  17. Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Urusula von der Leyen ametangaza wiki iliopita kwamba ameamuru meli hizo mbili kupelekwa bahari ya Mediterenia haraka iwezekanavyo.
  18. Amekaririwa akisema "hii ni mara ya kwanza kabisa kwamba tunachukuwa hatua kipau mbele kikiwa kuwasaidia watu walioko hatarini katika bahari ya Mediterenia na kuwaokowa wakimbizi wasizame."
  19. Rais Joachim Gauck wa Ujerumani ambaye amelifanya suala la hatima ya wakimbizi kuwa nukta muhimu katika agenda yake wakati bunge la Ujerumani likitafakari kumuongezea muhula wa pili madarakani amesema lengo la sera ya wakimbizi ya Umoja wa Ulaya linapaswa sio tu kulinda mipaka bali pia kulinda maisha ya watu wanaoingia ndani ya nchi hizo.
  20. Gauck alitowa kauli hiyo baada ya kutembelea hivi karibuni kituo cha wakimbizi karibu na mji mkuu Valetta wa kisiwa cha Malta ambacho kinawapa hifadhi wakimbizi kutoka Syria,Somalia, Eritrea na Sudan.
  21. Ufaransa na Uingereza ni miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya ambazo zimeahidi wakati wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya mwezi uliopita mjini Brussels kutuma meli zaidi bahari ya Mediterenia kusaidia kukabiliana na tatizo hilo la wakimbizi.Viongozi pia walikubali kuongeza mara tatu zaidi mchango wa kifedha kwa operesheni ya kulinda mipaka katika bahari ya Mediterenia ijulikanayo kama Triton.

0 comments: