Sunday, June 14, 2015

MTU mmoja amefariki dunia na wengine 28 kuheruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya Mafinga, mjini Iringa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutangata kupita daladala na kugongana na fuso, katika eneo la Kisolanza, Wilayani Mufindi.
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Iringa, Ramadhani Mungi alisema tukio hilo limetokea leo, majira ya saa nne asubuhi, wakati basi hilo aina ya Another G, likisafiri kutoka mjini Iringa kwenda Mbeya.
Amemtaja aliyefariki kuwa ni utingo wa fuso, ambaye jina lake halijapatikana na kuwa majeruhi wane hali zao mbaya wamekimbizwa hospitali ya rufaa ya Mafinga

0 comments: