Maofisa
wa ulinzi nchini marekani wamekiri kuwa maabara kadhaa zilizopokea
kimakosa sampuli hai za vidudu hatari vya kimeta ni zaidi ya mara mbili
ya matarajio ya awali.
Pentagon imesema vifaa hamsini na moja
katika majimbo kumi na saba nchini Marekani, pamoja na maabara zilizopo
nchini Canada, Australia na Korea kusini walitumiwa sampuli hizo kutoka
maabara ya jeshi la marekani.Imesema usafirishaji wa vijidudu hivyo vilianza miongo kadhaa iliiyopita na iliendelea mpaka wiki iliyopita.
Hadi sasa hakuna mtu aliyeathirika lakini zaidi ya watu ishirini walikuwa wakibeba sampuli hizo wamekuwa wakitibiwa kwa tahadhari tu.
0 comments:
Post a Comment