Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya karne moja, noti mpya ya dola kumi nchini Marekani itakuwa na picha na mwanamke.
Wizara
ya Fedha ya Marekani imewataka wananchi wa Marekani kutoa mawazo yao ni
picha ya mwanamke gani ichapishwe kwenye noti hiyo.Wizara hiyo imesema inatafuta kile kinachoelezwa kuwa demokrasia shirikishi.
Kwa sasa noti za Benki Kuu ya Marekani zilizo katika mzunguko wa fedha zinawaonyesha viongozi wa zamani wa kisiasa----wote wakiwa wazungu.
Noti hiyo mpya ya dola kumi itatolewa mwaka 2020 kuadhimisha miaka mia moja ya wanawake wa Marekani kupata haki ya kupiga kura.
0 comments:
Post a Comment