Tuesday, June 16, 2015

Marekani inasema itatoa msaada wa dola milioni 3.2 kufadhili kikosi cha kijeshi cha kimataifa kilichoundwa kukabiliana na wanamgambo wa Nigeria wa kundi la kiislamu la Boko Haram.
Naibu waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani anayehusika na maswala ya Afrika Thomas Greenfield, alisema Boko Haram si kero na tatizo tu kwa Nigeria bali kwa jumuiya ya kimataifa.
Msaada huo unatangazwa baada ya ziara ya rais Buhari kwenye kikao cha mataifa yenye utajiri mkubwa duniani maarufu kama G7 nchini Ujerumani, ambako alisema Nigeria inahitaji msaada zaidi wa kigeni kukabiliana na wanamgambo hao wa kiislamu.

Kundi hilo la kiislamu limelaumiwa kwa mauaji ya kujitoa mhanga yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 20 katika taifa jirani la Chad siku ya jumatatu.
null

Viongozi wa mataifa ya Magharibi mwa Afrika waliounda kikosi cha kuikabili Boko Haram
Chad itakuwa mwenyeji wa kikosi hicho kinachoongozwa na Nigeria chenye wanajeshi 7,500 kilichoundwa na mataifa matano.
Kuanzishwa kwa kikosi hicho kumepata msukumo upya baada ya rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kushika hatamu za uongzoi mwezi uliopita wa mei.
Uongozi wa awali chini ya Goodluck Jonathan ulionekana kutotilia maanani uundwaji wa kikosi hicho kwa hofu kwamba Nigeria huenda ingepoteza hadhi yake kama taifa huru.
Mwaka jana, Marekani ilikataa kuiuzia Nigeria silaha kwa sababu ya madai ya ukikwaji wa haki za kibinadamu na jeshi la nchi hiyo.
null

Boko Haram ilianza miak 6 iliyopita na imesababisha vifo vya watu elfu 13 na wengine milioni moja u nusu kuachwa bila makao.
Swala hili lilisababisha mzozo wa kidiplomasia, huku Nigeria ikishtumu Marekani kwa kile ilichokitaja kama
"kukataa kutoa msaada wa ambaoungetokomeza kabisa kundi la Boko Haram"
Umoja wa Afrika uliunga mkono kubuniwa kwa kikosi cha pamoja cha mataifa mapema mwaka huu, na kusema Boko Haram wanahitaji juhudi, maarifa na nguvu za pamoja kuwashinda.
Ukatili wa Boko Haram ambao ulioanza miaka 6 iliyopita umesababisha vifo vya watu elfu 13 na wengine milioni moja u nusu kuachwa bila makao.

0 comments: