Thursday, June 18, 2015

Umoja wa mataifa umesema kuwa idadi ya watu waliolazimishwa kukimbia makao yao kutokana na vita au tishio la kuuawa imefika juu zaidi kuliko miaka yote.
Takriban milioni sitini wamerekodiwa mwaka uliopita.
Zaidi ya nusu ya wakimbizi wote ni watoto.

null
Mlipuko huu wa wakimbizi kwa kiasi kikubwa umetajwa kusababishwa zaidi na machafuko nchini Syria.
Mjumbe wa masuala ya wakimbizi katika Umoja wa mataifa Antonio Guterres, amesema kuwa nchi nyingi zimeanzisha vita bila kujali matokeo yake na jamii ya kimataifa imesalia kutazama tu bila kuzuia ghasia.

0 comments: