Mwezi mtukufu wa Ramadhan unapoanza,
hospitali nchini Uingereza zinawasihi Waislamu kuchangia viungo vyao
kwa wagonjwa ambao wanahitaji figo au maini.
Kuna zaidi ya
Waislamu milioni 2.7 nchini Uingereza, na wale ambao wanahitaji figo au
maini hulazimika kugonja kwa muda mrefu zaidi kuliko wale ambao si
waislamu.Hii ni kwa sababu ya ukosefu wa wafadhili wanaofaa, tatizo ambalo haliwaathiri waingereza pekee.
Huyo ni Daktari Adnan Sharrif akizungumza na kijana mmoja mgonjwa Muislamu katika kitengo cha madakatari wa figo, hospitali ya Queen Elizabeth, Birmingha.
Nazma anafanyiwa matibabu ya figo, utaratibu ambao yeye hufanyiwa mara tatu kwa wiki kwa ajili ya ugonjwa ulioathiri figo yake.
Anahitaji figo, lakini kulingana na Daktari, atangoja angalau miake miine ndiposa aweze kupata figo inayomfaa, hapa ni suala la kupata figo yenye maumbile yanayoambatana na yake
''Bila shaka wagonjwa wetu watangoja kwa muda mrefu kupata matibabu, baadhi ya wagonjwa wengi wetu wa kiislamu wataaga dunia kama bado wako katika orodha ya wale wanaongoja figo, na idadi hiyo kwa maoni yangu inaongezeka''alisema Daktari Sharif.
Kote nchini Uingereza, Waislamu hasa wenye asili ya Asia hungoja mwaka mmoja hata zaidi ili kupata viungo kama figo na maini kuliko watu wasio waislamu.
Hospitali ya Malkia Elizabeth inajaribu kushawishi waislamu zaidi wajaribu kuchangia viungo hivi muhimu wakiwa hai ama waruhusu viungo vya wapendwa wao wanaofariki kutumika.
Ni swala nyeti mno, na waislamu wengi wanajadili ingawa Uislamu unakubali au unalaani kitendo hicho.
Hakuna ilikoandikwa katika kitabu kitakatifu cha Quran na wasomi nao wana maoni tofauti.
Daktari Yasser Mustapha ni mkufunzi ambaye huzuru misikiti kuzungumuzia swala hili la viungo vya maiti.
''Bila kujali asili ya Muislamu, awe kutoka afrika, Asia ama nwenye asili ya Uingereza, mara kwa mara hatimaye sote hujiuliza swali moja tu!
Ambalo wangependa jibu
''je viongozi wa dini ya kiislamu wanasema nini kuhusu utoaji msaada wa viungo?
0 comments:
Post a Comment