Wednesday, June 17, 2015



 
Mamlaka ya Chad imepiga marufuku vazi la Burqa kufuatia visa vya walipuaji wa kujitolea muhanga siku ya jumatatu ambavyo vimewaua watu 23.
Waziri mkuu Kalzeube Pahimi Deubet, alitangaza baada ya kuonana na viongozi wa kidini.
Amelaumu kundi la Boko Haram kwa kutekeleza mashambulizi huku kundi hilo likiendelea kuwatumia wanawake kama walipuaji wa kujitolea muhanga kwa kuwa ni rahisi wao kutotambulika.
Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Ndjamena tangu milipuko hiyo ambayo iliyalenga makao makuu ya polisi pamoja na chuo cha kutoa mafunzo ya polisi katika mji huo.

0 comments: