Watu 23 wameuawa Kaskazini mwa
Nigeria wakati mabomu yaliyokuwa yameachwa nyuma na wapiganaji wa kundi
la kigaidi la Boko Haram yalipolipuka katika kambi yao ya zamani.
Wapiganaji
wa kiraia wanaosaidiana na Serikali kupambana na Boko Haram walikuwa
wakipekua kambi hiyo iliyokuwa imehamwa na wapiganaji wa Boko Haram
karibu na mji wa Monguno wakati milipuko ilipotokea.Inadaiwa kuwa watu hao walikuwa wakisherehekea baada ya kupata mabomu hayo wakati ambapo bomu moja lililipuka na kusababisha madhara hayo makubwa.
Tukio hilo linaonyesha baadhi ya matatizo ambayo raia wanaendelea kukabiliana nayo hata wakati Boko Haram wanapoendelea kutimuliwa.
0 comments:
Post a Comment